Table of Contents
Kila mwaka, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), huchapisha majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati. Kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026, wanafunzi kutoka mkoa wa Dodoma wanataegemea kupata nafasi katika shule mbalimbali za sekondari na vyuo vya kati nchini.
Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 katika mkoa wa Dodoma yatapatikana kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI mara baada ya kutangazwa rasmi na TAMISEMI. Orodha hii inajumuisha wanafunzi kutoka halmashauri zote za mkoa wa Dodoma, ikiwa ni pamoja na:
- Bahi DC
- Chamwino DC
- Chemba DC
- Dodoma CC
- Kondoa DC
- Kondoa TC
- Kongwa DC
- Mpwapwa DC
1 Mchakato wa Uchaguzi wa Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati 2025 katika Mkoa wa Dodoma
Mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati umehusisha hatua kadhaa muhimu:
- Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne: Wanafunzi wanaofanya vizuri katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne hupewa kipaumbele katika uchaguzi wa kujiunga na kidato cha tano au vyuo vya kati.
- Upendeleo wa Mwanafunzi: Wanafunzi hupewa fursa ya kuchagua shule au kozi wanazopendelea kupitia mfumo wa uchaguzi wa shule na kozi.
- Upatikanaji wa Nafasi: Uchaguzi unategemea upatikanaji wa nafasi katika shule na vyuo mbalimbali, pamoja na vigezo vingine kama vile jinsia na mahitaji maalum.
- Uchambuzi na Uthibitisho: Baada ya kukusanya taarifa zote, TAMISEMI hufanya uchambuzi na kuthibitisha uchaguzi kabla ya kutangaza majina ya waliochaguliwa.
2 Sifa na Vigezo vya Wanafunzi Kuchaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati 2025 Mkoa wa Dodoma
Kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano au chuo cha kati, wameweza kufikia vigezo vifuatavyo:
- Ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne: Mwanafunzi anapaswa kuwa na alama zinazokidhi viwango vilivyowekwa na Wizara ya Elimu kwa ajili ya kujiunga na kidato cha tano au kozi za vyuo vya kati.
- Upendeleo wa Kozi au Shule: Uchaguzi wa mwanafunzi unazingatia upendeleo wake wa shule au kozi alizochagua wakati wa kujaza fomu za uchaguzi.
- Mahitaji Maalum: Wanafunzi wenye mahitaji maalum au wanaotoka katika makundi maalum wanaweza kupewa kipaumbele kulingana na sera za elimu za nchi.
- Usawa wa Jinsia: Serikali inahakikisha usawa wa kijinsia katika mchakato wa uchaguzi, hivyo basi idadi sawa ya wavulana na wasichana hupata nafasi za kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati.
3 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo 2025 Mkoa wa Dodoma
Ikiwa wewe ni mzazi au mwanafunzi, unaweza kufuatilia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati mwaka 2025 kwa kufuata hatua zifuatazo:
Hatua ya 1: Kutembelea Tovuti Rasmi ya TAMISEMI ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati
- Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha tano na vyuo vya kati kupitia https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/.
- Bofya linki ya “Form Five First Selection, 2025”.
Hatua ya 2: Chagua Linki ya Mkoa Ulikosoma (Mkoa wa Dodoma)
- Baada ya kufungua linki ya “Form Five First Selection, 2025”, utakutana na orodha ya mikoa yote Tanzania.
- Chagua mkoa wa Dodoma.
Hatua ya 3: Chagua Linki ya Halmashauri Ulikosoma
- Baada ya kufungua linki ya Mkoa wa Dodoma, utakutana na orodha ya halmashauri zote katika mkoa husika, ambazo ni:
- Bahi DC
- Chamwino DC
- Chemba DC
- Dodoma CC
- Kondoa DC
- Kondoa TC
- Kongwa DC
- Mpwapwa DC
- Chagua halmashauri ambayo mwanafunzi alifanyia mtihani wake wa kidato cha nne.
Hatua ya 4: Chagua Shule Uliyosoma
- Baada ya kufungua linki ya halmashauri husika, utakutana na orodha ya shule zote katika halmashauri hiyo.
- Chagua shule ambayo mwanafunzi alifanyia mtihani wake wa kidato cha nne.
Hatua ya 5: Angalia Orodha ya Majina na Pakua Maelekezo ya Kujiunga (Joining Instructions PDF)
- Baada ya kuchagua shule, utaweza kuona orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa pamoja na shule walizopangiwa.
- Pia, unaweza kupakua maelekezo ya kujiunga (joining instructions) ya shule husika katika mfumo wa PDF kupitia linki ya jina la shule mbele ya namba na jina la mwanafunzi.
Hatua ya 6: Kuhakikisha Taarifa
- Hakikisha unachunguza majina kwa umakini ili kuthibitisha kama mwanafunzi amechaguliwa na wapi.
Ikiwa kuna matatizo yoyote au maswali zaidi, unashauriwa kuwasiliana na ofisi za elimu za mkoa wa Dodoma au kutumia namba za msaada zilizotolewa katika tovuti husika.
4 Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo 2025 Mkoa wa Dodoma Kupitia Linki za Halmashauri Zote
Hapa chini ni orodha ya halmashauri za mkoa wa Dodoma pamoja na linki za kuangalia majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati:
Halmashauri | Linki ya Majina ya Waliochaguliwa |
Bahi DC | Bahi DC Selection |
Chamwino DC | Chamwino DC Selection |
Chemba DC | Chemba DC Selection |
Dodoma CC | Dodoma CC Selection |
Kondoa DC | Kondoa DC Selection |
Kondoa TC | Kondoa TC Selection |
Kongwa DC | Kongwa DC Selection |
Mpwapwa DC | Mpwapwa DC Selection |