wajanjaforum.com
No Result
View All Result
Subscribe
wajanjaforum.com
No Result
View All Result
wajanjaforum.com
No Result
View All Result
TAMISEMI Waliochaguliwa Kidato cha Tano

TAMISEMI Waliochaguliwa Kidato cha Tano

TAMISEMI Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 – Selection Form Five 2025 to 2026

Wajanjaforum by Wajanjaforum
April 3, 2025
in Selections, Articles
Reading Time: 7 mins read
0
Share on FacebookShare on Twitter

Table of Contents

  • 1. Mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2025
  • 2. Sifa za Wanafunzi Kuchaguliwa kidto cha tano kwa mwaka 2025
  • 3. Tarehe Muhimu za katika mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi kidato cha tano
  • 4. Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2025 Hatua kwa Hatua
  • 5. Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2025 Kupitia Orodha ya Mikoa

Uteuzi wa wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka 2025/2026, unajulikana kama “Selection Form Five 2025 to 2026,” ni mchakato wa kuwachagua wanafunzi ambao wamekidhi vigezo vya kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali za sekondari nchini Tanzania.

Uchaguzi wa kidato cha tano ni tukio muhimu katika mfumo wa elimu nchini Tanzania. Ukiwa na Lengo kuu la kuwawezesha wanafunzi waliomaliza mtihani wa kidato cha nne kuendelea na elimu ya juu (Kidato cha Tano na Cha sita).

Related Posts

Form Five Selection 2025 Tabora

Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Tabora – Form Five Selection 2025 Tabora

April 3, 2025
Form Five Selection 2025 Songwe

Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Songwe – Form Five Selection 2025 Songwe

April 3, 2025

Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Singida – Form Five Selection Singida 2025

April 3, 2025
Form Five Selection Simiyu

Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Simiyu – Form Five Selection Simiyu 2025

April 3, 2025

Uchaguzi wa kidato cha tano hufanyika kila mwaka ili kuchagua wanafunzi wenye ufaulu wa juu na kuwapa nafasi za kusoma masomo ya kidato cha tano na cha sita. Huu ni mchakato wa kiserikali unaosimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, pamoja na Vyuo vya Elimu ya Ufundi. Mchakato wa form five selection unaratibiwa na serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Wizara ya Elimu.

Mchakato wa uchaguzi unaanza na tathmini ya matokeo ya kidato cha nne. Vigezo vikuu ni ufaulu wa wanafunzi katika mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari (Kidato cha nne) na nafasi zilizopo katika shule na vyuo. Uchaguzi huu huwapa wanafunzi fursa ya kujiunga na kidato cha tano au kozi za elimu ya ufundi.

Uchaguzi huu una umuhimu mkubwa katika safari ya kielimu ya mwanafunzi kwa kuwa ndicho huwapa fursa ya kuendelea na masomo ya juu zaidi. Kwa muda mrefu, mchakato huu umechukuliwa kama kipimo cha mafanikio ya elimu ya msingi na sekondari, ukitoa nafasi kwa wale wenye alama za juu kujiunga na masomo ya ngazi inayofuata .

1 Mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2025

Mchakato wa uteuzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2025 unasimamiwa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Zoezi hili linahusisha kuchagua wanafunzi waliokidhi vigezo vya ufaulu na kuwapangia katika shule mbalimbali za serikali na vyuo vya elimu ya ufundi. Uchaguzi huu unazingatia ufaulu wa wanafunzi katika mtihani wa kidato cha nne. 

Alama za ufaulu ndizo kigezo kikuu kinachotumiwa kuamua wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano. Kwa mwaka 2025, wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la I hadi III ndiyo wanapewa kipaumbele kikubwa. Kwanza, watahiniwa wote walioandikishwa wanafanyiwa tathmini ya matokeo yao kidato cha nne 2024 na orodha ya wanafunzi waliochaguliwa hutolewa na kutangazwa rasmi.

2 Sifa za Wanafunzi Kuchaguliwa kidto cha tano kwa mwaka 2025

Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano unategemea kwa kiasi kikubwa sifa na vigezo vilivyowekwa na serikali na taasisi zake za elimu. Kwa mwaka 2025, zoezi la kuwapanga wanafunzi katika shule mbalimbali litategemea vigezo vitakavyozingatia ufaulu wa wanafunzi, nafasi zilizopo na mahitaji maalum ya wanafunzi.

Viwango vya Ufaulu

Kigezo kikuu cha kupata nafasi katika kidato cha tano ni ufaulu mzuri kwenye mtihani wa kidato cha nne. Watahiniwa wanaotegemewa wanatoka katika shule za serikali na zisizo za serikali, na pia watahiniwa wa kujitegemea ambao wana alama za kutosha katika madaraja ya I hadi III.

Mahitaji Maalum

Serikali inaangazia zaidi usawa wa kijinsia na inaweka kipaumbele kwenye kuandaa nafasi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum. Kwa mfano, mwaka 2024, wanafunzi 812 wenye mahitaji maalum waliteuliwa, hali inayotarajiwa kuendelea kwa mwaka 2025. Hii inaonyesha nia ya serikali ya kuwapa fursa sawia wanafunzi wote bila ubaguzi.

Usawa wa Kijiografia

Pia, kuna juhudi za kuweka usawa katika uteuzi kwa kuzingatia maeneo mbalimbali nchini. Mikoa inahimizwa kuwa na tahasusi zote za msingi katika shule zake ili kuhakikisha wanafunzi wanafaulu wanaweza kupata nafasi karibu na nyumbani, hivyo kuwapunguzia gharama za usafiri na kuimarisha ufanyaji wa masomo.

Fursa kwa Wanafunzi wenye alama za Juu

Kwa wanafunzi waliopata alama za juu, huchaguliwa kwenye shule zinazopokea wanafunzi wenye ufaulu wa juu, kama vile Kilakala, Mzumbe, na Ilboru. Hii inalenga kuwaandaa kwa masomo ya juu zaidi na kuwapa motisha ya kuendelea kufanya vizuri.

3 Tarehe Muhimu za katika mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi kidato cha tano

Mchakato wa uteuzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano unategemea ratiba rasmi inayotolewa na serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Wizara ya Elimu. Mchakato wa kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano unaanza na Kutangazwa kwa Matokeo ya Kidato cha Nne mwezi Januari, Majina ya waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano hutolewa mwishoni mwa mwezi Mei au mwanazo mwa mwezi Juni kila mwaka kupitia tovuti rasmi za TAMISEMI na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi (NACTVET) na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)

4 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2025 Hatua kwa Hatua

Ikiwa wewe ni miongoni mwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2024 na wanakidhi vigezo vya kujiunga na kidato cha tano mwaka 2025, ufuatao ni mwongozo wa  jinsi ya kuangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2025.

Hatua ya 1: Tembelea Tovuti Rasmi

  • Ingia kwenye tovuti rasmi ya TAMISEMI selform ambayo ni https://selform.tamisemi.go.tz/Account/Login 

Hatua ya 2: bofya kwenye linki ya slection 

  • Ndani ya tovuti hiyo, tafuta kiungo au sehemu iliyoandikwa “Selection Results“. Baada ya kubofya kwenye linki hiyo utapelekwa kwenye ukurasa maalum wa Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati

Hatua ya 3: Nenda kwenye Selection Details na Ingiza Taarifa Muhimu       

  • Baada ya kuingia kwenye ukurasa wa Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati, utaweza kuingiza namba ya mtihani ya mwanafunzi ( F4 IndexNo eg. S0001.0101.2024) ili kupata matokeo ya shule aliyopangiwa. Hakikisha kuwa unayo namba sahihi ya mtihani.

Hatua ya 4: Kuangalia Orodha Ya Waanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati

  • Kupata orodha kamili ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa pamoja na shule walizopangiwa bofya linki ya First Selection, 2025. Chagua mkoa, wilaya husika na shule uliyosoma ili kupata orodha ya waliochaguliwa.

5 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2025 Kupitia Orodha ya Mikoa

Kama mzazi au mwanafunzi, unaweza kufuatilia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2025 kwa kupitia lnki maalum za mikoa. Zifuatazo ni hatua za kufuata:

Hatua ya 1: Kutembelea Tovuti Rasmi ya TAMISEMI ya Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati

  • Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI ya Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati kupitia https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/ 
  • Bofya linki ya  form five First Selection, 2025

Hatua ya 2: Chagua Linki Ya Mkoa Ulikosoma

  • Baada ya kufungua linki ya form five First Selection, 2025, utakutana na orodha ya mikoa yote tanzania,
  • Chagua mkoa ambao mwanafunzi amefanyia mtihani wake wa kidato cha nne.

Hatua ya 3: Chagua Linki Ya Halmashauri Ulikosoma

  • Baada ya kufungua linki ya Mkoa ulikosoma, utakutana na orodha ya Halmashauri zote katika mkoa husika,
  • Chagua halmashauri ambayo mwanafunzi amefanyia mtihani wake wa kidato cha nne.

Hatua ya 4: Chagua Shule Uliyosoma

  • Baada ya kufungua linki ya Halmashauri ulikosoma, utakutana na orodha ya shule zote katika Halmashauri husika,
  • Chagua shule ambayo mwanafunzi amefanyia mtihani wake wa kidato cha nne.

Hatua ya 5: Angalia Orodha ya Majina na Pakua Maelekezo ya kujiunga (Joining instructions pdf)

  • Baada ya kuchagua shule, unaweza kupata orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa pamoja na shule walizopangiwa. Pia unaweza kupakua joining instruction ya shule husika (kama PDF) kupitia linki ya Jina la shule husika mbele ya Namba na Jina la Mwanafunzi

Hatua ya 6: Kuhakikisha Taarifa

  • Hakikisha unachunguza majina kwa umakini ili kuthibitisha kama mwanafunzi amechaguliwa na wapi.

Ikiwa kuna matatizo yoyote au maswali zaidi, unashauriwa kuwasiliana na ofisi za elimu za mkoa husika au kutumia namba za msaada zilizotolewa katika tovuti husika.

Tarehe ya Kuripoti Shuleni: Wanafunzi wanapaswa kuanza kuripoti katika shule zilizopangiwa kuanzia tarehe 30 Juni na tarehe ya mwisho ya kuripoti ni 14 Julai.

Maelekezo ya Namna ya Kujiunga: Unaweza kupakua joining instruction ya shule husika (kama PDF) kupitia linki ya Jina la shule husika mbele ya Namba na Jina la Mwanafunzi

Soma makala hizi pia

  • Majina Ya Waliochaguliwa Kujiunga Na Vyuo Vya Kati 2025/2026 - Selection Za Vyuo 2025/26
ShareTweetPin
Previous Post

Majina Ya Waliochaguliwa Kujiunga Na Vyuo Vya Kati 2025/2026 – Selection Za Vyuo 2025/26

Next Post

Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Tanga – Form Five Selection 2025 Tanga

Wajanjaforum

Wajanjaforum

Related Posts

Form Five Selection 2025 Tabora
Articles

Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Tabora – Form Five Selection 2025 Tabora

April 3, 2025

Kila mwaka, matokeo ya uteuzi wa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha tano nchini Tanzania...

Form Five Selection 2025 Songwe
Selections

Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Songwe – Form Five Selection 2025 Songwe

April 3, 2025

Kila mwaka, idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha nne husubiria kwa hamu kubwa...

Articles

Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Singida – Form Five Selection Singida 2025

April 3, 2025

Kila mwaka, baada ya matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne kutangazwa,...

Form Five Selection Simiyu
Articles

Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Simiyu – Form Five Selection Simiyu 2025

April 3, 2025

Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa inayotarajia kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi...

Next Post
Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Tanga – Form Five Selection 2025 Tanga

Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Tanga – Form Five Selection 2025 Tanga

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

  • About Us – WajanjaForum
  • Home

© 2025 WajanjaForum - Karibu kwenye tovuti ya Wajanjaforum.

No Result
View All Result
  • About Us – WajanjaForum
  • Home

© 2025 WajanjaForum - Karibu kwenye tovuti ya Wajanjaforum.