Kila mwaka, wanafunzi wanaofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne wanachaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya kati. Kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026, mkoa wa Mwanza umejipanga kutoa nafasi kwa wanafunzi waliofaulu ili kuendelea na masomo ya sekondari ya juu na mafunzo ya kati.
Mchakato huu unaendeshwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, ukihusisha kuorodhesha wanafunzi kulingana na ufaulu wao katika mtihani wa kidato cha nne.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo 2025 Mkoa wa Mwanza
Kama mzazi au mwanafunzi, unaweza kufuatilia majina ya waliopata nafasi kwa kupitia njia za mtandaoni. Zifuatazo ni hatua rahisi unazoweza kutumia kuangalia majina hayo:
Hatua ya 1: Kutembelea Tovuti Rasmi ya TAMISEMI ya Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati
Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI kupitia hii linki.
Hatua ya 2: Chagua Linki Ya Mkoa Ulikosoma (Mkoa wa Mwanza)
Baada ya kufungua tovuti, chagua linki ya form five First Selection, 2025 na kisha uchague mkoa wa Mwanza.
Hatua ya 3: Chagua Linki Ya Halmashauri Ulikosoma
Baada ya kufungua linki ya mkoa wa Mwanza, utapata orodha ya Halmashauri zote katika mkoa husika, ambazo ni:
- Buchosa DC
- Ilemela MC
- Kwimba DC
- Magu DC
- Misungwi DC
- Mwanza CC
- Sengerema DC
- Ukerewe DC
Hatua ya 4: Chagua Shule Uliyosoma
Chagua halmashauri ambayo mwanafunzi amefanyia mtihani wake na kisha shule ambayo mwanafunzi amefanyia mtihani wake wa kidato cha nne.
Hatua ya 5: Angalia Orodha ya Majina na Pakua Maelekezo ya Kujiunga (Joining instructions pdf)
Baada ya kuchagua shule, utaona orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa, pamoja na shule walizopangiwa. Unaweza pia kupakua maelekezo ya kujiunga kwa shule husika.
Hatua ya 6: Kuhakikisha Taarifa
Hakikisha unachunguza majina kwa umakini ili kuthibitisha kama mwanafunzi amechaguliwa na wapi. Ikiwa kuna matatizo yoyote au maswali zaidi, unashauriwa kuwasiliana na ofisi za elimu za mkoa wa Mwanza au kutumia namba za msaada zilizotolewa katika tovuti husika.
Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo 2025 Mkoa wa Mwanza kupitia Linki za Halmashauri Zote
Halmashauri |
Buchosa DC |
Ilemela MC |
Kwimba DC |
Magu DC |
Misungwi DC |
Mwanza CC |
Sengerema DC |
Ukerewe DC |