Kila mwaka, idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha nne husubiria kwa hamu kubwa majina ya kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati nchini Tanzania. Hii ni fursa kubwa kwa wanafunzi kujiendeleza kielimu katika mwelekeo wa taaluma zao. Mkoa wa Songwe, ambao umekuwa ukikua kwa kasi, pia unashuhudia ongezeko la idadi ya wanafunzi ambao wanastahili kuchaguliwa. Kujua majina ya waliochaguliwa ni jambo muhimu kwa wanafunzi na wazazi wa wanafunzi kwaajili ya kujiandaa na hatua inayofuata ya elimu.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo 2025 Mkoa wa Songwe
Orodha Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa katika Mkoa wa Songwe inajumuisha wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati kwa mwaka 2025/2026.
Ikiwa unahitaji kufuatilia majina haya kwa urahisi. Unaweza kufanya hivi kwa kutembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI na kuzingatia hatua kadhaa zilizopendekezwa.
Hatua ya 1: Kutembelea Tovuti Rasmi ya TAMISEMI
Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI kwa kupitia hapa.
Hatua ya 2: Chagua Linki ya Mkoa wa Songwe
Baada ya kufungua link ya “Form five First Selection, 2025”, utaona orodha ya mikoa yote. Chagua mkoa wa Songwe.
Hatua ya 3: Chagua Halmashauri
Kwenye mkoa wa Songwe, utaona halmashauri zifuatazo:
- Ileje DC
- Mbozi DC
- Momba DC
- Songwe DC
- Tunduma TC
Chagua halmashauri ambayo mwanafunzi amefanyia mtihani.
Hatua ya 4: Chagua Shule Uliyosoma
Baada ya kuchagua halmashauri, utapata orodha ya shule. Chagua shule yako ilikofanyika mtihani.
Hatua ya 5: Angalia Orodha na Pakua Maelekezo
Orodha ya majina ya wanafunzi na shule walizopangiwa itapatikana, pamoja na maelekezo ya kujiunga.
Hatua ya 6: Kuhakikisha Taarifa
Hakikisha kuwa unachunguza majina kwa umakini ili kuthibitisha kama mwanafunzi amechaguliwa na wapi.
Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo 2025 Mkoa wa Songwe
Halmashauri | Linki ya Kucheki |
Ileje DC | Tazama hapa |
Mbozi DC | Tazama hapa |
Momba DC | Tazama hapa |
Songwe DC | Tazama hapa |
Tunduma TC | Tazama hapa |
Ikiwa umechaguliwa kujiunga na chuo cha kati, hakikisha umepata fomu zote muhimu za kujiunga pamoja na vifaa vya masomo. Ni muhimu kuzingatia tarehe za kuripoti na maelekezo mengine yaliyo kwenye fomu za maelekezo.