Table of Contents
Kila mwaka, baada ya matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne kutangazwa, wanafunzi wengi husubiri kwa hamu kujua kama wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano au vyuo vya kati. Ni muhimu kwa wanafunzi na wazazi kuangalia majina ya waliochaguliwa ili kupanga hatua zinazofuata katika safari ya elimu. Mara tu baada ya Majina ya waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya kati kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 kutangazwa mapema mwezi Mei, wazazi na wanafunzi wataweza kuangalia majina hayo kupitia tovuti ya NACTVET na TAMISEMI.
1 Mchakato wa Uchaguzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati 2025
Mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati kwa mwaka 2025 unahusisha hatua kadhaa muhimu. Baada ya matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne 2024 kutangazwa tarehe 23 Januari 2025 , wanafunzi walipewa fursa ya kuchagua tahasusi na vyuo wanavyopendelea kupitia mfumo wa Selform wa TAMISEMI. Uchaguzi huu ulizingatia alama za mwanafunzi, uchaguzi wa tahasusi, na nafasi zilizopo katika shule au vyuo husika. Serikali, kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI, imehakikisha kuwa mchakato huu umefanyika kwa haki na uwazi, ili kila mwanafunzi apate nafasi inayostahili kulingana na ufaulu wake.
2 Sifa za na vigezo vya Wanafunzi Kuchaguliwa Vyuo Vya Kati 2025
Ili mwanafunzi achaguliwe kujiunga na vyuo vya kati kwa mwaka 2025, anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne: Wanafunzi waliopata alama za juu, hasa wale wenye Daraja la Kwanza hadi la Tatu, wana nafasi kubwa ya kuchaguliwa.
- Uchaguzi wa vyuo Kupitia mfumo wa Selform, wanafunzi waliochagua tahasusi wanazopendelea na vyuo. Uchaguzi sahihi wa vyuo huongeza uwezekano wa kuchaguliwa.
- Nafasi Zilizopo: Idadi ya wanafunzi wanaochaguliwa inategemea nafasi zilizopo katika vyuo husika. Hivyo, hata kama mwanafunzi amefaulu vizuri, uchaguzi wake unaweza kuathiriwa na upatikanaji wa nafasi.
- Maadili na Nidhamu: Wanafunzi wenye rekodi nzuri ya nidhamu na maadili mema shuleni wana nafasi nzuri ya kuchaguliwa, kwani vyuo vinathamini tabia njema pamoja na ufaulu wa kitaaluma.
3 Tarehe Rasmi ya Kutangazwa kwa Majina ya Uchaguzi wa Wanafunzi Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati
Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 yanatarajiwa kutangazwa mwezi Mei au Juni 2025. Hata hivyo, tarehe halisi inaweza kutofautiana kulingana na mchakato wa uchambuzi na maandalizi. Ni muhimu kwa wanafunzi na wazazi kufuatilia tovuti rasmi za TAMISEMI na NACTE kwa taarifa za uhakika na za hivi karibuni kuhusu mchakato huu.
4 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo Vya Kati 2025/2026
Baada ya majina ya waliochaguliwa kutangazwa, unaweza kufuata hatua zifuatazo kuangalia kama umechaguliwa:
- Tembelea Tovuti Rasmi ya TAMISEMI au NACTE: Fungua kivinjari chako na uende kwenye tovuti rasmi ya TAMISEMI (https://selform.tamisemi.go.tz) au NACTE (https://www.nacte.go.tz).
- Tafuta Sehemu ya Selection Results: Katika ukurasa wa mbele wa tovuti, tafuta kiungo au sehemu iliyoandikwa “Selection Results”.
- Bofya kwenye linki ya slection : Ndani ya tovuti hiyo, tafuta kiungo au sehemu iliyoandikwa “Selection Results“. Baada ya kubofya kwenye linki hiyo utapelekwa kwenye ukurasa maalum wa Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati
- Nenda kwenye Selection Details na Ingiza Taarifa Muhimu:Baada ya kuingia kwenye ukurasa wa Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati, utaweza kuingiza namba ya mtihani ya mwanafunzi ( F4 IndexNo eg. S0001.0101.2024) ili kupata matokeo ya shule aliyopangiwa. Hakikisha kuwa unayo namba sahihi ya mtihani.
- Kuangalia Orodha Ya Waanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati: Kupata orodha kamili ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa pamoja na shule walizopangiwa bofya linki ya First Selection, 2025. Chagua mkoa, wilaya husika na shule uliyosoma ili kupata orodha ya waliochaguliwa.
5 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo 2025 Kupitia Orodha ya Mikoa
Kama mzazi au mwanafunzi, unaweza kufuatilia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo mwaka 2025 kwa kupitia lnki maalum za mikoa. Zifuatazo ni hatua za kufuata:
Hatua ya 1: Kutembelea Tovuti Rasmi ya TAMISEMI ya Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati
- Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI ya Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati kupitia https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/
- Bofya linki ya form five First Selection, 2025
Hatua ya 2: Chagua Linki Ya Mkoa Ulikosoma
- Baada ya kufungua linki ya form five First Selection, 2025, utakutana na orodha ya mikoa yote tanzania,
- Chagua mkoa ambao mwanafunzi amefanyia mtihani wake wa kidato cha nne.
Hatua ya 3: Chagua Linki Ya Halmashauri Ulikosoma
- Baada ya kufungua linki ya Mkoa ulikosoma, utakutana na orodha ya Halmashauri zote katika mkoa husika,
- Chagua halmashauri ambayo mwanafunzi amefanyia mtihani wake wa kidato cha nne.
Hatua ya 4: Chagua Shule Uliyosoma
- Baada ya kufungua linki ya Halmashauri ulikosoma, utakutana na orodha ya shule zote katika Halmashauri husika,
- Chagua shule ambayo mwanafunzi amefanyia mtihani wake wa kidato cha nne.
Hatua ya 5: Angalia Orodha ya Majina na Pakua Maelekezo ya kujiunga (Joining instructions pdf)
- Baada ya kuchagua shule, unaweza kupata orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa pamoja na shule walizopangiwa. Pia unaweza kupakua joining instruction ya shule husika (kama PDF) kupitia linki ya Jina la shule husika mbele ya Namba na Jina la Mwanafunzi
Hatua ya 6: Kuhakikisha Taarifa
- Hakikisha unachunguza majina kwa umakini ili kuthibitisha kama mwanafunzi amechaguliwa na wapi.
Ikiwa kuna matatizo yoyote au maswali zaidi, unashauriwa kuwasiliana na ofisi za elimu za mkoa husika au kutumia namba za msaada zilizotolewa katika tovuti husika.
6 Nini kinafuata Baada ya Kuchaguliwa Kujiunga na Vyuo Vya Kati
Ikiwa umechaguliwa kujiunga na chuo cha kati, ni muhimu kuchukua hatua zifuatazo:
- Pakua fomu ya maelekezo ya Kujiunga: Kupitia tovuti ya chuo husika au TAMISEMI, pakua na uchapishe joining instructions forms inayotoa maelekezo muhimu kuhusu tarehe ya kuripoti, mahitaji ya chuo, na mengineyo.
- Andaa Mahitaji Muhimu: Hakikisha unapata sare za chuo, vifaa vya masomo, ada, na mahitaji mengine kama ilivyoelekezwa kwenye barua ya kujiunga.
- Ripoti kwa Wakati: Fika chuoni kwa tarehe iliyopangwa ili kuepuka kufutiwa nafasi yako. Kutoshiriki kwa wakati kunaweza kusababisha kupoteza nafasi yako.
- Fuatilia Taarifa za Ziada: Endelea kufuatilia tovuti rasmi za chuo na TAMISEMI kwa taarifa zozote mpya au mabadiliko yanayoweza kutokea.